Tumeweka mkazo sana juu ya kile ambacho taifa linaweza kufanyia kila mmoja wetu - haki zetu - na kusahau kile ambacho kila mmoja wetu anapaswa kufanyia taifa letu. Yafuatayo ni mapendekezo muhimu yaliyotolewa na Jopokazi:

  1. Wakenya wana haki kutoka kwa Mungu ambazo sasa ni lazima ziende sambamba na Mkataba wa Majukumu ya Wananchi ambayo yamehamasishwa na Wimbo wa Kitaifa na Maadili ya Kitaifa, na inajumuisha Ahadi ya Uzalendo kwa Taifa na Katiba ya Kenya (kwa shule, mahali pa kazi na katika hafla rasmi za kitaifa na umma).

  2. Kuanzisha na kuendesha mipango ya kuendeleza na kusambaza elimu ya uraia kuhusu haki na majukumu.

  3. Fundisha watoto utamaduni wa uwajibikaji kwa kubuni mipango ya utendaji na kujitolea shuleni ili kusaidia jamii na asasi zilizo karibu na shule.

  4. Kuwatiisha Mawaziri wote na Makatibu Wakuu kwa taasisi za umma wanazoendesha. Ikiwa asasi za umma haziwafai, basi wao hawawafai Wakenya.

  5. Kubuni mtaala wa kulea watoto na kufundisha ulezi katika asasi za kidini, vituo vya afya na katika asasi nyinginezo za kijamii, serikali na kitamaduni.

  6. Kuhimiza vijana Wakenya kati ya miaka 18 hadi 26 kujitolea kwa kipindi cha miezi sita ya maisha yao kuwatumikia Wakenya kwa hiari.