Search

Stori Ya Influencer Kevo

Updated: Feb 13, 2020


Kevo ameishi kukopa ‘Tara’ ndo alipe ‘MSwali’. Mimi nikicheki call yake najuanga tu ni reverse call na anadai kunikopa doh. Kuna day nilichukua tenje yake na kupitia twitter feed. Manze sijai ona msee anachukia gava kama yeye. Kwanza kuna moja niliona akidai ati hizo locust zilicome Kenya zilitumwa na Prophet Owuor zikam kufunza gava adabu.

Keja ya Kevo ni self-contained na huwa anaiita kichinjio. Siko sure ni nini huwa anachinja huko, labda ni vile ye hujikatia Sukuma na kukatakata tule tunyama twa soo ndo tukue tudogo. Although mara mob ye hukula hapo kwa mathee. Ye husema anasupport local businesses but najua ni doh humsumbua tu. Akiwa mafutani, utampata akidishi food za ma Bombay.


Unaona, Kevo alimaliza chuo kama two years ago but hajawahi works. Ye husema tenje yake ndo job yake. Huwa analipwa kumanage social media za businesses na kupush hashtags zitrend on twitter. Anajiitanga influencer but sidhani kama amefika hio level bado. Buda ako na chocha mob sana.


Juzi tulikuwa tunachana base, zilishika nikauliza Kevo anaweza taka nini ihappen tutoke situation ya kusota na kuwa hopeless. Sikuwahi dhani Kevo ako mbright hivo. Alidai, ati hizi company za kubet zinampea false hopes.


‘Aiii aje bro? Si nadhani hapo ndo we hupata kakitu?’ nikamuuliza.


‘Ziii! Cheki siezi ishi nikiekelea bet za 50 bob kila saa nihope nitacome kuget 100K! Alafu unajua nyinyi ndo hunichocha kubet hata, hio doo afadhali nieke bank izaane nifungue kabizna hivi’ akanijibu.

Kiasi akadai ati angepata msee wa kumpea advice fiti angekuwa anarun malls ka kumi hivi. Okay, hapo ali exaggerate but niliget point yake. Imagine tungezoeshwa kuwa na mind set ya kufanya biz tukiwa watoi?


‘Na huwa unalipa tax bro?’ nikamuuliza.


“Acha hizo, tax nalipa tu nikibuy vitu…hio ingine ni ya masonko bana, but unajua gava ingetutolea hizo ma tax mob za kuanzisha biz, ningekuwa narun company ya social media management. Kwanza mathee angekuwa na ka grocery store ya gorofa mtu wangu.” akasema akicheka.


Nilicheki Kevo, nikaona ile knowledge huyu boy ako nayo akitoboa tuneza shangaa. “Bro, unaonaje hii stori ya BBI?” Nikaona ni mtest kidogo.


Kevo akatema taxin, akachukua maji akaosha mdomo na kujipaka Vaseline kwa lips. Akachukua miwani zake akavaa alafu akaniangalia huku amegeuza sura akakaa serious.


‘Acha nikushow bro,’ akasema,” “Hio kitu sisi hatudai, hawa mapolitician wanataka tu kutukulia”

“Wanatukulia nini?” nikamuuliza.


“Si unacheki vile wao hubehave manze, siezi watrust mimi. Badala wa address vitu tunadai wao wako mdomo za siasa tu.”


Hapa nilijua nilikuwa nimemget vizuri. “Hehe, bro, na si hizo vitu zote umesema unataka zichange kwa country ziko kwa hio BBI report.” Actually, BBI inadai ukifungua biz ka youth, unafaa usilipe tax the first seven years. Kevo akaniangalia chini ya miwani ka buda mzee.


“Kuwa serious? Yani miaka saba bila tax si nitajenga biz fiti?”. Akanigota juu ya hiyo point ya biz. “Na hao politicians wanatubeba za ovyo na pesa zetu?” Nikashow Kevo, “Kuna vile BBI inasema tudeal nao. Tunawachuja ofisi, kuchukua doh na properties wamenunua through corruption alafu tunawatupa Kamiti ki bazenga”


Kevo akarelax, nikaona amesmile, “Wallahi! Unamaanisha chenye nimekuwa nikiona kwa mneti ni chocha tu?”


“Bro, wewe ni influencer, si unajua watu hulipwa kuchocha watu kwa mtandao? Do hivi, nenda kwa official handle ya BBI ujisomee hizo matweets,” Nikamshow. Kevo alichukuwa tenje akaingia tweet feed ya BBI. Nikaona amescroll kiasi halafu msee akasimama akiruka!


“Yoooo! Hawa wasee wanatweet hadi na sheng’? Aaah kwanza hapa acha niwapee follow ju ya hio stori. Btw hizi recommendations ni poa, hazikai zile uwongo nimekuwa nikiona! Brathee thanks sana umeniokolea. Acha hata niretweet hizi stuff zinanice na pia nitacomment vitu nadai waongeze”


Apart from kutushika hio day, Kevo alishika kitu important. Chenye tunadai ihappen haiko mbali, iko kwa hio report ya BBI. Tuwache kuignore stuff na tuisome vizuri. Majob, opportunities, education fiti, health safi na kuongeza tusmile huku na kule, tunahitaji kukaa sote tudiscuss vile tuta achieve. Tuache kudangaywa na watu online, sisi wenyewe tumake our own decisions. Sisi tu ndo tuneza leta hio change.


Kesho kuna form Kevo ameniitia ya kucheki vile tunaweza shika wasee majani chai safi imetoka highlands za Rift Valley. Haikosi zilishika kuruka. Naona hii BBI ishaanza kuchocha life ya Kevo. Bro, Sis, download hiyo report pale www.bbi.go.ke na ucheki form ni gani.

281 views0 comments