01

Masuala Muhimu

Wanajopo wa BBI walipokuwa wanazunguka nchini, waligundua matatizo makubwa ambayo yanaathiri suluhisho zilizobainishwa kukabiliana na changamoto maalum. Wanatoa wito kwa kila mmoja kutafakari kwa kina zaidi ikiwa kweli tunataka ufumbuzi wa changamoto zetu zingine ili kujenga Kenya yenye umoja, amani na mafanikio.

02

Maadili ya Kitaifa

Tunakosa imani, maadili na matamanio ya pamoja kuhusu nini Kenya inaweza kuwa ikiwa sote tutazingatia maadili ya kitaifa ambayo hujenga na kuimarisha umoja wetu. Utaratibu huu ni fursa ya kihistoria kwetu kuanza, kwa hiari, kufafanua, kuendeleza na kuyaambata maono ya pamoja ambayo yataleta umoja Kenya na uwezo wa kukabili changamoto zake zote kuu.Hii ni kazi ya ujima, inayoanzia katika familia na jamii, ikisaidiwa na mikakati inayokumbatia tamaduni nzuri, imani na maadili ya jamii mbalimbali za Kenya na kuwezeshwa na mashirika ya kijamii, sekta ya kibinafsi, na asasi za Serikali. Itajumuishwa katika mfumo rasmi wa elimu, kuanzia chekechea na kudumu milele, asasi za dini na utamaduni, vyombo vya habari, na sekta yetu ya sanaa. Hayatakuwa maadili ya jamii moja bali ya jamii zenye sauti tofautitofauti zilizomotishwa na hamu ya kuchangia, kumiliki na kujenga taifa ambalo ni nyumbani kwetu sote. Hapa chini ni baadhi ya mapendekezo muhimu zaidi ambayo wanajopo wanaamini yatasaidia kujenga maadili thabiti ya kitaifa.

03

Majukumu na Haki za Uraia

Tumeweka mkazo sana juu ya kile ambacho taifa linaweza kufanyia kila mmoja wetu - haki zetu - na kusahau kile ambacho kila mmoja wetu anapaswa kufanyia taifa letu. Yafuatayo ni mapendekezo muhimu yaliyotolewa na Jopokazi:

04

Uhasama wa Kikabila na Ushindani

Haya ndio matishio makuu kwa ufanisi wa Kenya na ustawi wa nchi yetu. Jopokazi linapendekeza hatua zifuatazo zichukuliwe:

05

Chaguzi zenye kuleta Migawanyiko

Jopokazi linapendekeza mfumo ambao utashughulikia mahitaji yetu ya kipekee, hususan katika kuunda mfumo wa ndani ya nchi au wa kiasili utakaolainisha mamlaka makuu ya nchi na uwakilishi.

06

Ushirikishwaji

Jopokazi linatoa mapendekezo makuu katika kuimarisha ushirikishwaji kwa misingi ya kisiasa, kiuchumi, kijamii, kidini, kitamaduni, vijana, na kijinsia. Hapa kuna baadhi yake

07

Ustawi kwa Wote

Tunahitaji mapinduzi ya kiuchumi, ili kujenga uchumi ambao unaweza kuzalisha kazi tunazohitaji, haraka. Wakenya walioongea katika kila kikao cha mashauriano kinachoendeshwa na Jopokazi, katika kila Kaunti, walizungumzia matatizo yao yanayochangiwa na umaskini na ukosefu wa kazi au ajira za mapato duni. Changamoto moja muhimu inayokabili Wakenya kuhusu suala la ustawi wa pamoja ni kuunda kazi za kutosha na ajira, haswa kwa vijana. Haitoshi tu kuboresha uchumi wetu na kupanua uwekezaji: ni lazima tuibadilishe kabisa mfumo wa uendeshaji wa uchumi wetu ikiwa tunataka kukabiliana na ukosefu wa kazi uliopo sasa. Baadhi ya Mapendekezo machache makuu katika ripoti ni: 

08

Ufisadi

Dhana iliyokita mizizi miongoni mwa Wakenya kwamba kuwa na serikali inayotawala kiharamu huwatuza wandani wake nyadhifa serikalini na kuendeleza ufisadi, kinyume na utendakazi bora na bidii, ndilo tishio kuu kwa utangamano na usalama.  Jopokazi linatoa mapendekezo makuu na yenye kutekelezeka, baadhi yake yametajwa hapa chini.

09

Ugatuzi

Kuhusu suala la kuondoka mamlakani baada ya utawala wa nchi na usimamizi wa rasilimali za umma, ugatuzi umekuwa na ufanisi mkubwa. Hata hivyo, ugatuzi bado unazongwa na changamoto tele ambazo ikiwa hazitatafutiwa ufumbuzi, kutaibuka maswali kuhusu uendelevu wake kisiasa na kiuchumi. Mapendekezo makuu yaliyotolewa na Jopokazi ni pamoja na yafuatayo:

10

Usalama na Ulinzi

Wakenya waliambia Wanajopo kwamba hawajisikii salama. Jopokazi lilibaini kwamba Kenya iko katika eneo hatari na vitisho vya ugaidi vinavyozidi kujitokeza, mataifa yenye utawala unaoyumba au dhaifu na nchi zenye mizozo ya kimipaka, unyanyasaji wa polisi na matendo haramu ya kijambazi yanayokiuka haki za binadamu. Jopokazi linapendekeza hatua madhubuti zifuatazo:

11

Tume na Masuala Yanayogusa kila kipengee

Jopokazi linapendekeza;