Dhana iliyokita mizizi miongoni mwa Wakenya kwamba kuwa na serikali inayotawala kiharamu huwatuza wandani wake nyadhifa serikalini na kuendeleza ufisadi, kinyume na utendakazi bora na bidii, ndilo tishio kuu kwa utangamano na usalama.  Jopokazi linatoa mapendekezo makuu na yenye kutekelezeka, baadhi yake yametajwa hapa chini.

 1. Komboa Kenya kutokana na wakiritimba kupitia mikakati ya kuvunja miungano wa wakiritimba na kuwaadhibu wahusika ipasavyo.

 2. Kuhimiza ufichuaji wa ufisadi kwa kuwapa wanaofichua shughuli za ufisadi asilimia 5 ya pesa zilizorejeshwa.

 3. Kuwalinda wafichuzi wa ufisadi - Wezesha taratibu za mahakama ambazo zinahakikisha usalama na ulinzi kwa watoaji habari, wafichuzi na mashahidi, hususan kuhusu ugaidi, uhalifu mkubwa wa kimataifa, na ufisadi.

 4. Piga marufuku watumishi wote wa umma kufanya biashara na serikali. Pia hawapaswi kujihusisha na biashara nje ya serikali isipokuwa ikiwa shughuli wanazotaka kujihusisha nazo zinaidhinishwa.

 5. Fanya fomu zote za kutangaza mali ziwe wazi kwa umma.

 6. Fanya Kenya iwe nchi inayotoa huduma kupitia mfumo wa elektroniki kwa asilimia 100 kwa kuweka kidijitali huduma zote za serikali, michakato, mfumo wa ulipaji na uwekaji wa rekodi.

 7. Zidisha imani ya raia kwa Idara ya Mahakama kwa kutambua kuwa mihimili mikuu ya katiba nchini Kenya ni kutenganisha mamlaka, kati ya vitengo vikuu vya Serikali, na uwajibikaji kwa Wakenya. Ni sharti uhuru wa Mahakama ulindwe kama mhimili mkuu, lakini nayo pia inapaswa kuwajibikia Wakenya.

 8. Ili kuimarisha mchakato wa kuyajibu malalamishi katika mahakama, Ofisi ya Wakili wa Wananchi inahitaji mageuzi ili iweze kufikiwa na umma na kushughulikia haja zao.

 9. Linda uhuru wa vyombo vya habari ili kufichua ufisadi lakini hakikisha kuwa madai ya uwongo na kuharibu jina hakutatizi utoaji wa huduma kwa watu.

 10. Tumia mbinu ya kuzuia na kukatisha tamaa kwa kuhakikisha kuwa umma umehamasishwa vyema kuhusu maadili kupitia mafunzo na elimu, kuwatuza wafichuzi wa ufisadi na kutathmini utendakazi.

 11. Punguza ubadhirifu na uozo katika Mashirika ya Serikali wa kuwa wasimamizi wasiojali wakitarajia dhamana ya Serikali kwa hatua zifuatazo:

 • Kuimarisha uwezo wa Mdhibiti wa Bajeti ili aweze kugundua mapema na kushughulikia kwa wakati unaofaa matumizi mabaya ya pesa, ubadhirifu, na michakato iliyo haramu.

 • Kama Rais alivyoamrisha mnamo Novemba 2015, lainisha mashirika ya umma kwa kujikita zaidi kwenye lengo la kimsingi la shirika husika na kupunguza ubadhirifu wa fedha kwa kutunga Mswada wa Mageuzi ya Mashirika ya Umma.