Jopokazi linatoa mapendekezo makuu katika kuimarisha ushirikishwaji kwa misingi ya kisiasa, kiuchumi, kijamii, kidini, kitamaduni, vijana, na kijinsia. Hapa kuna baadhi yake:

  • Mwandishi Maalum wa Masuala ya Ushiriki wa Umma— Kuimarisha ubora, uwazi, na ushirikishwaji katika michakato ya ushiriki wa umma unaohitajika Kikatiba kwa kubuni Ofisi ya Mwandishi Maalum wa kushughulikia Ushiriki wa Umma. Ofisi hiyo itapewa jukumu la kuandaa shughuli za kuushirikisha umma kwa niaba ya taasisi zote za serikali na zisizo za serikali zinazotekeleza mipango ya sera na utendaji ambayo, Kikatiba, inahitaji ushiriki wa umma. Mwandishi Maalum wa Masuala ya Ushiriki wa Umma anapaswa kuweka rekodi sahihi kuhusu ushiriki wa umma hadharani na aweze kukidhi haja za asasi zinazotaka huduma yake. Kando na jukumu la kuimarisha uwazi na kufanikisha ushiriki wa umma, ongezea ofisi hiyo jukumu ambalo litasababisha ubishi kuhusu maslahi ya umma kwa namna ambavyo inakingwa dhidi ya ushawishi wa msambazaji/mchuuzi. Mfano wa jinsi jambo hili linaweza kufanya kazi katika mfumo wa demokrasia unapatikana katika kielelezo cha India.

  • Jamii zilizotengwa hazifai kuwatenga wengine— Ithibati kutokana na mashauriano ya BBI katika kaunti inaonyesha maoni yenye uzito kwamba baadhi ya jamii ambazo zililalamika kuhusu kutengwa katika ngazi ya kitaifa zenyewe zilikuwa na hatia ya kutenga jamii za watu wachache katika Kaunti husika. Kwa hivyo ilikuwa wazi kuwa mageuzi ya kukuza ushirikishwaji katika ngazi ya kitaifa yanapaswa pia kuonekana katika kiwango cha Kaunti.

  • Uraia wa mataifa mawili - Kuhusu suala la Wakenya walio na uraia wa mataifa mawili kuwa wasioaminika kwa msingi huo, huo unakuwa ubaguzi na kiwango ulinzi na utambulisho wao unarudi chini. Wakenya walio tayari kuwa watumishi wanapaswa kupimwa kwa vigezo vya tabia na utendakazi wao mzuri na si kudhaniwa kuwa wamegawa uaminifu wao kuwili, ambao unatia doa maadili na uzalendo wao. Kwa hivyo, mipaka ya uwezo wa raia wa mataifa mawili kuwahudumia Wakenya unapaswa kuwa mdogo zaidi. Mfano mmoja ni kuhusu vikosi vya ulinzi, ambavyo kikatiba vinaweza kuamrishwa kushambulia wanajeshi wa nchi nyingine ambazo vikosi hivi vinaweza kuwa na uraia nazo. Kwa kuzingatia uchunguzi huu, Jopokazi linapendekeza kwamba watumishi pekee wa Serikali wanaoweza kuwekewa mipaka ya kuwa na uraia wa mataifa mawili wawe Amiri Jeshi Mkuu wa Kikosi cha Ulinzi, wanachama wa vikosi vya ulinzi, na uanachama wa Baraza la Ulinzi.